From e9f82ccaf095eb14191d599b0580e477dc5a3ee8 Mon Sep 17 00:00:00 2001 From: mihaipopahtp Date: Wed, 17 Jul 2024 21:08:25 +0300 Subject: [PATCH 1/2] HTP; common_voice_privacy_notice.md/common_voice_terms.md --- sw/common_voice_privacy_notice.md | 27 +++++++++++ sw/common_voice_terms.md | 80 +++++++++++++++++++++++++++++++ 2 files changed, 107 insertions(+) create mode 100644 sw/common_voice_privacy_notice.md create mode 100644 sw/common_voice_terms.md diff --git a/sw/common_voice_privacy_notice.md b/sw/common_voice_privacy_notice.md new file mode 100644 index 00000000..6bd015ef --- /dev/null +++ b/sw/common_voice_privacy_notice.md @@ -0,0 +1,27 @@ +# Taarifa ya Faragha ya Mradi wa Common Voice + +Ilianza kutumika tarehe 27 Juni 2024 {: datetime="2024-06-27" } + +## Faragha + +Wakati Mozilla (ambayo ni sisi), inapokea maelezo yako, [Sera yetu ya Faragha ya Mozilla](https://www.mozilla.org/privacy) inaeleza jinsi tunavyoshughulikia maelezo hayo. + +* **Data binafsi.** Unaweza kututumia kwa hiari yako maelezo kama vile lugha, umri na jinsia yako. Hii hutusaidia sisi pamoja na watafiti wengine kuboresha na kubuni teknolojia na zana za kunukuu matamshi. + +* **Data ya akaunti.** Si lazima ufungue akaunti ili utumie Common Voice. Ukiamua kufungua akaunti, tutapokea jina la mtumiaji na picha yako ya ishara, iwapo utawasilisha. Anwani yako ya barua pepe inahusishwa na data yako binafsi na utumiaji lakini haitolewi hadharani. Tunaonyesha bao za wanaoongoza zinazoonyesha idadi ya rekodi ambazo watumiaji hutayarisha. Unaweza kuamua iwapo ungependa kuonekana kwenye bao za wanaoongoza au la. Unaweza kufuta akaunti yako wakati wowote na jina la mtumiaji na barua pepe yako vitaondolewa. + +* **Anwani ya barua pepe.** Ukishiriki katika majaribio ya Alpha au Beta ya mradi wa Common Voice Spontaneous Speech, ni lazima uweke anwani yako ya barua pepe ili tuweze kukutumia kiungo cha kuingia ili ushiriki katika mradi wa Common Voice Spontaneous Speech. Unaweza kufungua akaunti kamili wakati wowote(kama ilivyobainishwa hapo juu). Iwapo hutafungua akaunti kamili baada ya kukamilisha majaribio ya Alpha au Beta, tutafuta anwani yako ya barua pepe ndani ya wiki mbili baada ya kukamilika kwa kila mpango wa kujaribu. Aina fulani za ushiriki katika jaribio la Beta (kwa mfano kwa lugha zenye nyenzo chache mno) huenda zisihitaji kuingia kwa kutumia anwani ya barua pepe. + +* **Jarida.** Unaweza kufuatilia jarida letu, ambapo tutapokea anwani yako ya barua pepe. Unaweza kujiondoa wakati wowote na anwani yako ya barua pepe yako itaondolewa kwenye orodha ya usambazaji wa jarida. + +* **Rekodi za Sauti.** Rekodi za sauti, pamoja na data yoyote binafsi iliyotolewa kwa hiari, vinaweza kupatikana katika hifadhidata ya mradi wa Common Voice kwa matumizi ya umma na matumizi ya jumla chini ya Leseni ya Creative Commons Zero ([CC0](https://creativecommons.org/publicdomain/zero/1.0/)). + +* **Maandishi.** Ukiwasilisha sentensi zilizoandikwa, tunaweza pia kuzifanya zipatikane katika hifadhidata za mradi wa Common Voice kwa matumizi ya umma chini ya [CC0](https://creativecommons.org/publicdomain/zero/1.0/), kulingana na sampuli zetu zote. Hatutahusisha sentensi hizi na data binafsi unayowasilisha. + +* **Data ya matumizi.** Tunatumia teknolojia ya Google Analytics ili kuelewa vyema jinsi unavyotumia programu au tovuti ya mradi wa Common Voice. Kwa mfano, tunaweza kutumia vidakuzi kufuatilia maelezo yasiyokutambulisha kama vile idadi ya sampuli za sauti unazorekodi au kusikiliza, vitendo unavyofanya kupitia vitufe na menyu na urefu wa kipindi. + +* **Data ya kiufundi.** Tunatumia teknolojia ya Google Analytics ili kuelewa vyema jinsi unavyotumia programu au tovuti ya mradi wa Common Voice. Kwa mfano, tunaweza kutumia vidakuzi kufuatilia maelezo yasiyokutambulisha kama vile idadi ya sampuli za sauti unazorekodi au kusikiliza, vitendo unavyofanya kupitia vitufe na menyu na urefu wa kipindi. Pia tunakusanya URL na kichwa cha kurasa za Common Voice unazotembelea. Ili kuendelea kuboresha hali ya utumiaji wa mradi wa Common Voice, tunakusanya maelezo kuhusu aina na toleo la kivinjari, ukubwa wa eneo la kutazama na ubora wa skrini. Hii inatuwezesha tuelewe jinsi watu wanavyotumia Common Voice ili tuweze kuiboresha. Pia tunakusanya maelezo ya mahali ulipo, na mipangilio ya lugha katika kivinjari chako ili kuhakikisha inakufaa. Ikiwa ungependelea kujiondoa katika shughuli ya ukusanyaji wa data ya Google Analytics, unaweza kuweka programu-jalizi ya [Google Analytics Opt-out Browser Add-on](https://tools.google.com/dlpage/gaoptout), ambayo huzuia data isitumwe kwa Google Analytics. + +[Pata maelezo zaidi](https://github.com/common-voice/common-voice/blob/main/docs/data_dictionary.md) + + diff --git a/sw/common_voice_terms.md b/sw/common_voice_terms.md new file mode 100644 index 00000000..ecb522ee --- /dev/null +++ b/sw/common_voice_terms.md @@ -0,0 +1,80 @@ +# Masharti ya Kisheria ya Mradi wa Common Voice + +Ilianza kutumika tarehe 27 Juni 2024 {: datetime="2024-06-27" } + +Kupitia mradi wa Common Voice, unaweza kuchangia sauti yako, sentensi zilizoandikwa na nyenzo zingine tunazohitaji kubuni hifadhidata huria ya sauti ambayo mtu yeyote anaweza kutumia kubuni programu bunifu za utambuzi wa sauti kwa vifaa na wavuti. + +Unaweza tu kushiriki katika mradi wa Common Voice ikiwa unakubali na Masharti haya ya Kisheria ya Common Voice (“Masharti”). + +## 1. Ustahiki + +Mradi wa Common Voice uko wazi kwa kila mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 19. Ikiwa una umri wa miaka 19 au chini yake, ni lazima uwe na idhini ya mzazi au mlezi na lazima wasimamie hali yako ya kushiriki katika mradi wa Common Voice. + +Mradi wa Common Voice ni sehemu ya Mozilla Community. Kwa hivyo, ukiamua kushiriki, unakubali kufuata [Mwongozo wa Kushiriki wa Mozilla Community](https://www.mozilla.org/about/governance/policies/participation/). + +## 2. Michango Yako + +Tunatoa hifadhidata ya mradi wa Common Voice wa Mozilla chini ya [kitengo cha kikoa cha umma cha CCO cha Creative Commons](https://creativecommons.org/publicdomain/zero/1.0/). Hiyo inaamanisha inapatikana hadharani na tumeondoa hakimiliki zote kadri tuwezavyo chini ya sheria. Ikiwa utashiriki katika mradi wa Common Voice, tutakutaka ufanye vivyo hivyo. Unakubali kuwa Mozilla inaweza kutoa hadharani michango yako yote kwenye mradi wa Common Voice, ikiwa ni pamoja na maandishi, rekodi, uthibitishaji na maoni (“Michango”) chini ya kitengo cha kikoa cha umma cha [CC0](https://creativecommons.org/publicdomain/zero/1.0/). + +Ili ushiriki katika mradi wa Common Voice, Mozilla pia inahitaji utoe uhakikisho wa mambo matatu: + +Kwanza, kwamba Michango yako ni kazi yako mwenyewe kabisa. + +Pili, kwamba Michango yako haikiuki haki zozote za washirika wengine. + +Tatu, kwamba Michango yako inatii [Sera ya Matumizi Yanayokubalika](https://www.mozilla.org/about/legal/acceptable-use/)ya Mozilla. + +Ikiwa huwezi kutoa uhakikisho mambo haya, hupaswi kushiriki katika mradi wa Common Voice. + +Zaidi ya hayo, ikiwa utashiriki katika mradi wa Common Voices Spontaneous Speech, unakubali kutojumuisha data yoyote nyeti au binafsi kukuhusu wewe na wengine katika rekodi unazowasilisha. + +## 3. Akaunti Yako + +Si lazima ufungue akaunti ili kushiriki katika mradi wa Common Voice. + +Ukifungua akaunti, Mozilla itaomba anwani yako ya barua pepe na jina la mtumiaji unalopendelea. Au, unaweza pia kuweka picha ya ishara na data fulani binafsi ambayo itatusaidia tuelewe jinsi ya kufundisha mashine kuelewa watu wa lugha, umri, jinsia na asili tofauti. + +Ukishiriki katika majaribio ya Alpha au Beta ya mradi wa Common Voice Spontaneous Speech, ni lazima utoe anwani yako ya barua pepe ili tuweze kukutumia kiungo cha kuingia ili ushiriki katika mradi wa Common Voice Spontaneous Speech. + +Unapotoa maelezo ya akaunti yako, unaipa Mozilla ruhusa zote zinazohitajika ili: kufuatilia maelezo kuhusu Michango yako, kuhusisha Michango hiyo na akaunti, anwani ya barua pepe, jina lako la mtumiaji na maelezo binafsi unayotoa, kuchapisha Michango yako hadharani pamoja na maelezo yoyote binafsi, na kuchapisha vipimo kuhusu Michango yako (kama vile idadi ya rekodi na lugha) pamoja na jina lako la mtumiaji kwenye ubao wa wanaoongoza. + +Mozilla haitachapisha au kutoa hadharani anwani yako ya barua pepe. + +Unaweza kuchagua kutoonekana kwenye bao za wanaoongoza. Ukifanya hivyo, Mozilla haitachapisha data kuhusu rekodi zako zinazohusiana na jina lako la mtumiaji. Hata hivyo, Mozilla bado itachapisha hadharani maandishi na rekodi zako kama sehemu ya mradi wa Common Voice na itajumuisha maelezo kuhusu rekodi zako katika vipimo vya jumla vinavyopatikana hadharani. + +## 4. Mawasiliano + +Iwapo utajisajili ili kupokea majarida yetu au ukifungua akaunti inayohusiana na mradi wa Common Voice, unaweza kupokea barua pepe kutoka kwetu kuhusiana na akaunti yako. + +## 5. Makanusho + +Kwa kushiriki katika mradi wa Common Voice, unakubali kwamba Mozilla haitawajibika kwa njia yoyote ile kwa kutoweza kutumia mradi wa Common Voice au kwa dai lolote litakalotokana na masharti haya. Mozilla inakanusha wazi yafuatayo: + +Uharibifu usio wa moja kwa moja, maalum, unaoambatana, unaotokana na, au wa adhabu, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, uharibifu wa moja kwa moja au usio wa moja kwa kupoteza nia njema, kusimamishwa kazi, kupoteza faida, kupoteza data au hitilafu ya kompyuta. + +Dhima yoyote ya Mozilla chini ya Masharti haya ni kima cha $500 pekee. + +Unakubali kufidia na kutowajibisha Mozilla kwa dhima au dai lolote linalotokana na kushiriki kwako katika mradi wa Common Voice. + +Mozilla inatoa mradi wa Common Voice “kama ulivyo.” Mozilla inakanusha wazi dhamana au mahakikisho yoyote kama vile “ubora kwa mauzo,” “ufaafu kwa kusudi fulani,” “kutokiuka,” na dhamana zinazotokana na shughuli, matumizi au biashara. + +## 6. Taarifa za Ukiukaji + +Ikiwa unahisi kuwa kitu fulani katika mradi wa Common Voice kinakiuka hakimiliki na haki za chapa ya biashara, tafadhali soma [sera yetu kuhusu jinsi ya kuripoti ukiukaji](https://www.mozilla.org/about/legal/report-infringement/). + +## 7. Masasisho + +Kila baada ya muda fulani, Mozilla inaweza kuamua kusasisha Masharti haya. Tutachapisha Masharti yaliyosasishwa mtandaoni. + +Iwapo utaendelea kutumia mradi wa Common Voice baada yetu kuchapisha Masharti yaliyosasishwa, unakubali kwamba hii inamaanisha kuwa unakubali mabadiliko hayo. Tutachapisha tarehe ya kuanza kutumika katika sehemu ya juu ya ukurasa huu ili kuweka wazi wakati ambapo tulifanya sasisho letu la hivi majuzi zaidi. + +## 8. Ukomeshaji + +Mozilla inaweza kusimamisha au kukomesha ufikiaji wa mtu yeyote wa mradi wa Common Voice wakati wowote kwa sababu yoyote. Tukiamua kusimamisha au kukomesha ufikiaji wako, tutajaribu kukuarifu kupitia anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako au wakati mwingine utakapojaribu kufikia mradi wa Common Voice. + +Michango unayowasilisha kwa Mozilla itaendelea kupatikana hadharani kama sehemu ya mradi wa Common Voice, hata tukikomesha au kusimamisha ufikiaji wako. + +## 9. Sheria Simamizi + +Sheria ya jimbo la California inatumika kwa Masharti haya. Masharti haya ni makubaliano yote kati yako na Mozilla kuhusu mradi wa Common Voice. + From 56485c8934a750c67e4e766673644d95bec40b91 Mon Sep 17 00:00:00 2001 From: Peiying Date: Wed, 17 Jul 2024 11:34:02 -0700 Subject: [PATCH 2/2] Update common_voice_terms.md --- sw/common_voice_terms.md | 2 +- 1 file changed, 1 insertion(+), 1 deletion(-) diff --git a/sw/common_voice_terms.md b/sw/common_voice_terms.md index ecb522ee..9e087ab9 100644 --- a/sw/common_voice_terms.md +++ b/sw/common_voice_terms.md @@ -22,7 +22,7 @@ Kwanza, kwamba Michango yako ni kazi yako mwenyewe kabisa. Pili, kwamba Michango yako haikiuki haki zozote za washirika wengine. -Tatu, kwamba Michango yako inatii [Sera ya Matumizi Yanayokubalika](https://www.mozilla.org/about/legal/acceptable-use/)ya Mozilla. +Tatu, kwamba Michango yako inatii [Sera ya Matumizi Yanayokubalika](https://www.mozilla.org/about/legal/acceptable-use/) ya Mozilla. Ikiwa huwezi kutoa uhakikisho mambo haya, hupaswi kushiriki katika mradi wa Common Voice.